MISHE-BOY

Sport | Huyu mchezaji Mugabo Prince ni Beki mzuri sana kwa kila mechi

Anaitwa Mugabo Prince ni beki wa timu ya Vital'o FC nchini Burundi, alijiunga na klabu hiyo msimu  huu 2017/2018 akitokea katika klabu ya Onze Rapide D'or.

Kati ya wachezaji  wenye vipaji vya soka hapa Burundi na Afrika Mashariki, Mugabo Prince ni mmoja wao.
Ni beki wa kati mzuri mwenye nguvu, akili, kujiamini na kujituma pia (central defender) pia anauwezo wakucheza kama beki wa kulia.

Amekuwa muhimu katika kikosi cha Vital'o FC kwenye mechi aliyoanza na kikosi, ata kama hapewi na fasi nyingi sana ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza, bado anaonekana bora zaidi.

Kwasasa beki huyu klabu za nje ya nchi zimeanza kumuwania na kumshawishi mchezaji aondoke na kujiunga na klabu izo uku beki huyu akiwataka waeshimu mkataba wake na Vitalo tu.

Hakuna maoni