MISHE-BOY

Sport | Moussa Mossi (Hadji) asimamishwa rasmi pamoja na wachezaji wengine wa 3

Kamati ya Mashindano ya Soka la FFB imetowa barua ya kujulisha klabu zinazoshiriki katika ligi la taifa ya Primus League msimu huu 2018-2019, kwamba kwa ombi la Kamati ya Kisheria ya FFB, mchezaji wa zamani wa LLB, Moussa Mossi akifahamika kwajina la Hadji Makoun haruhusiwi kushiriki katika mechi yoyote kwa muda mrefu mpaka atakapo rudisha ada ya uajiri ambazo alipewa na klabu nyingine ya Inter Stars.

Kiungo wa zamani wa klabu ya LLB na Vital'o FC, Moussa Mossi amepewa adhabu  Septemba 21 na Kamati ya Mashindano ya Soka la FFB, ya kutokucheza mechi yoyote msimu huu baada ya kukutwa na hatia ya kitendo cha kusaini mkataba katika klabu mbili tofauti msimu moja.

Moussa alisajiliwa na Inter Star klabu ambayo iliteremka daraja msimu uliyopita, baada ya kushiriki katika michezo ya kirafiki na klabu yake mpya hiyo, mchezaji huyu alionekana tena katika mchezo wa klabu ya daraja ya kwanza msimu, Les Lieres dhidi ya Musongati ya mkoani Gitega (1-1).

Halmashauri wa amana inayosimamia klabu ya soka ya Inter Stars, itaakayo shiriki Ligi B, imechukua hatua ya kupeleka malalamiko yao na kushinda huku kamati ya Mashindano ya FFB imechukua hatua ya kumsimamisha mchezaji huyo mpaka atakapo rudisha ada ya uajiri ambazo alipewa na klabu ya Inter Stars.

Aidha, wachezaji wengine ambao walikutwa na hatia hiyo hiyo na kupewa adhabu ya kusimamishwa ni pamoja na Ingabire Christie wa Aigle Noir, ambaye aliwai kusaini msimu huu na Olympic Star, Sibomana Abdoul wa Ngozi City, ambaye aliwai pia kusaini mkataba na Olympic Star, Ndori Israel alisajiliwa pia na Olympic Star na Moussa Mossi wa Les Lieres ambaye aliwai kusajiliwa na Inter Stars


Hakuna maoni